Mkongwe wa zamani wa washika bunduki wa jiji la London klabu ya Arsenal Thierry Henry alipata fursa ya kujumuika na kikosi chake zamani ambacho kipo jijini New York kwaajili ya kujifua na kujiweka fiti kwa msimu mpya wa ligi ya Uingereza 2014/2015.
Katika ziara hiyo Henry anayecheza klabu ya New York Red Bull kwasasa, alikuwa kama mwenyeji wa jiji katika kuhakikisha vijana wa mzee Wenger haingi katika vyoo vya kike.
Hapa Henry akijaribu kuwaonyesha kipaji watoto wa mzee Wenger, kwamba siyo soka tuu ndio mchezo anaoumudu.
Pia baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza akiwemo Jack Wilshire, Aaron Ramsey, Gibbs na Rosicky walipata nafasi ya kucheza basketball pamoja na legend wa klabu yao kama picha zinavyoonesha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni