Sports and Entertainment

Alhamisi, 31 Julai 2014

ISRAEL INAKIUKA SHERIA ZA KIMATAIFA

Hakuna maoni :
Mkuu wa haki za binaadam wa Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameituhumu Israel kwa kuvunja kwa makusudi sheria za kimataifa, katika harakazi zake za kijeshi Gaza. 

Bi Pillay amesema Israel inaweza ikatakiwa kuwajibika kwa uhalifu wa kivita kufuatia kushambulia shule, hospitali, makazi na hata ofisi za Umoja wa Mataifa.

 Pia ameishutumu Marekani kwa kushindwa kutumia uwezo wake juu ya Israel na kumaliza mapigano, na kuipa Israel silaha nzito zaidi kutumia. Msemaji wa shirila la kibinaadam la Umoja wa Mataifa, Chriss Guiness amesema imezidiwa na kiasi kikubwa cha hali ya kibinaadam iliyosababishwa na mzozo huo. Watu robo milioni kutoka Palestina wamepoteza makazi yao na wanatafuta hifadhi katika umoja huo.
LikeLike ·  ·  · 73940142

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni