Jumapili, 23 Novemba 2014
Kwa speed hii wanaijeria lazima wakae
Kwa mtazamo wetu, Afrika Mashariki haijawahi
kuwa na ushirikiano wa karibu kama tunaouona
sasa.
Hebu tuangalie kwa ufupi.. Turudi nyuma
hadi pale Victoria Kimani alipowashirikisha
Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz kufanya
wimbo Prokoto.
Shaa alichaguliwa na kituo cha Citizen TV kuwa
host wa show yao ya Sakata Mashariki na
kiukweli watazamaji wamempokeza vizuri.
Shaa huyo huyo pia amefanya collabo na Redsan
na mambo mengi yanakuja ikiwa ni pamoja na
uwezekano wa kufanya ngoma na Jacky Chandiru
wa Uganda.
Hivi karibuni tumeshuhudia picha za wasanii wa
Afrika Mashariki wakiwemo Shaa, AY, Maurice
Kirya, Jose Chameleone, Nameless, Rabbit, Erick
Wainaina na wengine walikutana jijini Nairobi
ambako kuna kitu kikubwa kinapikwa.
Weusi wamefanya remix ya Afrika Mashariki ya
wimbo wao Gere ambapo wamewashirikisha
Navio wa Uganda na Naziz na Collo wa Kenya. Ni
jana tu pia Navio ameingia studio kurekodi wimbo
alioshirikishwa na Izzo Bizness.
Hiyo haitoshi.. msanii wa Uganda, Zari the
Bosslady alikuja Tanzania na kufanya collabo na
Diamond Platnumz.
Bado kituo cha runinga cha Maisha Magic
kimeendelea kuja na vipindi vya kuwaungasha
wana Afrika Mashariki zaidi. Salama Jabir
ameungana na Mkenya, Malonzo kuwa hosts wa
kipindi cha Tujuane Plus.
Jokate Mwegelo ameungana na staa wa Uganda,
Gaitano Kagwa kuwa hosts wa show mpya, Beat
the Challenge.
Kwa mifano hiyo michache, utagundua jinsi
ambavyo Tanzania, Kenya na Uganda zinazidi
kuwa karibu katika sekta ya burudani. Hicho
ndicho kitu pekee ambacho tunaweza kufanikiwa
kuwa kwenye ligi moja ya kimuziki na wasanii wa
Nigeria.
Hatuwezi kuwafikia kama tutajitenga. Ushirikiano
ulioneshwa na wana Afrika Mashariki baada ya
kundi la Sauti Sol kuingia hatua ya pili kwenye
tuzo za MTV EMA ulivutia wengi. Ushirikiano huo
huo uendelee pale msanii wa Afrika Mashariki
anapokuwa akishindana na wasanii wa Nigeria.
Leo hii mafanikio ya Diamond Platnumz
hayasherehekiwi na Watanzania pekee. Ukiangalia
comments kwenye video zake, utaona meseji
nyingi kutoka kwa mashabiki wake wa Kenya
wanaojivunia mafanikio yao.
Nchi za Afrika Mashariki zinaunganishwa na
tamaduni nyingi lakini kikubwa ni Kiswahili
ambacho kinatufanya kuwa kitu kimoja.
Tukiendelea na mshikamano huu, tunaweza
kutengeneza industry ya burudani kubwa
itakayowanufaisha wasanii wa nchi zote. Afrika
Mashariki tuendelee kuungana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni