Alhamisi, 27 Novemba 2014
mpambano wa Mayweather na Pacquiao wazidi kunukia
Bondia nyota wa Marekani mwenye rekodi ya kutokupigwa hata pambano moja, Floyd Mayweather Jr. ameanza kuonyesha hofu juu ya pambano lake dhidi ya mhasimu wake mkubwa bondia mfilipino ‘Manny Pacquiao’ litakalochezwa hapo mwakani.
Katika ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na mtandao wa Daily Mail ilimnukuu mkufunzi wa Pacquiao, Freddie Roach akisema amekubaliana na ombi la Mayweather la kuwepo kwa kifungu cha pambano la marudiano ikiwa ni katika moja ya sharti alilotaka lizingatiwe.
”Ufahamu wangu ni kwamba Floyd anasisitiza juu ya pambano la marudiano endapo akipigwa na Pacquiao, ambapo naamini atapigwa. hiyo iko sawa kwetu”, alisema Roach.
Hii sio mara ya kwanza kwa Mayweather kusisitiza pambano la marudiano katika mikataba yake. Itakumbukwa Mwaka 2013, bingwa huyo wa Dunia alifanya kama kile alichofanya sasa kwa bondia Robert Guerrero katika mpambano uliopigwa kwenye ukumbi wa MGM Grand Arena ingawa alifanikiwa kushinda.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni