Jumamosi, 6 Desemba 2014
Tata Martino ajutia msimu wake mbaya Barca
Kocha wa zamani wa magwiji wa soka la Hispania, Barcelona ; Tata Martino amedai kwamba anajutia msimu mbaya aliokumbana nao wakati yuko katika klabu hiyo, Martino mwenye miaka 52 amesema kuwa licha ya kufanya kwake hovyo lakini angepewa muda hadi sasa mambo yangekuwa shwari Catalan
"Kutokana na mawasiliano yetu ya kwanza, ningefanya karibu kila kitu tofauti," aliiambia Marca.
"Mimi sikutoa mifano yoyote, lakini mimi najuta mambo mengi yaliyotokea wakati huo, ingawa wameweza imenisaidia kujifunza na si kurudia makosa kama hayo."
Kocha huyo wa zama ni wa Paraguay alikwenda mbele zaidi na kumpigia chapuo Leo Messi katika tuzo ya mchezaji bora wa Dunia na kusisitiza kuwa shirikisho la soka Duniani lifikirie tena juu ya tuzo hizo
"Baadhi ya makocha hawaangalii sana juu ya suala hilo," alisema.
"Mimi ni mmoja wao. Kama Messi ni katika anashindana, nataka ashinde. nitampigia kura yeye
Labda tunapaswa kufikiria upya juu ya nani anapiga kura kwa ajili ya tuzo hii. Kuna mambo mengi binafsi."
Hata hivyo Messi ambae hakushinda taji lolote msimu uliopita anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mshindi wa kombe la Dunia mlinda mlango Manuel Neuer pamoja na mtambo wa mabao wa mabingwa wa Ulaya Real Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo ambapo mshindi atatangazwa januari 12
No related posts
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni