Mkewe
Rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama alipowasili nchini Saudi
Arabia na mumewe bila ya kujitanda kichwa chake kwa kitambaa, wengi
walitarajia kwamba mitandao ya kijamii nchini humo ingewaka moto kwa
mingon'ono.
Ingawa vyombo kadhaa vya habari Ulaya, viliripoti kuhusu utata mkubwa kutokea kwenye mitandao ya kijamii, alama ya njia ya reli kwenye mtandao wa Twitter kwa lugha ya kiarabu...ikimaanisha ....''Michelle Obama bila mtandio''...ujumbe huo ilisambazwa kwenye mtandao huo zaidi ya mara 2,5000.
Hii sio idadi kubwa ya watu waliousambaza ujumbe huo lakini pia sio ndogo sana katika nchi yenye watumiaji wengi wa Twitter.
Pia inaarifiwa ujumbe huo ulizidiwa nguvu na ujumbe mwingine uliotumwa kwenye Twitter dhidi ya ziara ya Rais Obama nkatika ufalme huo.
''Mfalme Salman amwacha Obama na kwenda kuomba,'' huu ndio ulikuwa ujumbe mwingine uliosambazwa sana kwenye Twitter kuhusu ziara ya Obama nchini humo.
Ujumbe huo: "Mfalme Salman amwacha Obama na kwenda kuomba,'' uliwavutia zaidi ya watu 170,000.
''Huyu ndiye mwanamume aliyemwacha kiongozi wa nchi muhimu zaidi duniani akimsubiri wakati akienda kusali'', aliandika mtu mmoja kwenye mtandao wa Twitter.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni