Timu ya Celtic ya Scotland iliambulia kichapo cha mabao 4-1dhidi ya wenyeji wao Legia Warsaw ya Poland .
Kocha wa Celtics Ronny Deila alikuwa amefungua kampeini yake ya mkondo wa tatu ya kufuzu kwa kombe la mabingwa barani Ulaya kwa kishindo na bao la mapema la Callum McGregor.
Hata hivyo vigogo hao wa ligi ya Scotland hawakuamini macho yao Miroslav Radovic alipoifungia Legia Warsaw bao la kufana la kusawazisha na hivyo bao la ufunguzi wa kichapo hicho.
Radovic alivunja mioyo ya Celtics alipofunga bao la pili kabla ya mapumziko.
Celtics yambulia kichapo Poland
Masaibu ya Celtics yaliongezeka Efe Ambrose alipoonyeshwa kadi nyekundu kwa kucheza visivyo.
Nusura kichapo hicho kisalie kuwa cha aibu lakini Ivica Vrdoljak alikosa mikwaju mwili ya penalti lakini Michal Zyro na Jakub Kosecki walitamatisha kichapo hicho cha kihistoria.
Celtics bado ina matumaini ya kuendelea katika ligi ya mabingwa ila kwa kikwazo kimoja tu- kuibuka mshindi na mabao 3-0 huko Murrayfield, Jumatano, wiki ijayo.
Hakuna aliyetarajia hilo jinsi mambo yalivyobadilika dhidi ya Celtics lakini bila shaka mchezaji McGregor aling’aa katika mchuano huo sawa na raundi iliyopita wakiwa Iceland.
Kwa mtizamo mmoja kupoteza kwa Celtics ni mwiba wa kujidunga kwani punde tu baada ya kupata bao lao la kwanza, hawakulinda ngome yao.
Ambrose akitimuliwa uwanjani
Kocha Deila amekubali kuwa walishindwa kustahimili upinzani.
Safu yetu ya Ulinzi ilivuja mara nyingi sana na hivyo tunakibarua kigumu katika mkondo wa pili''.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni