Mlinzi kisiki wa Ureno anaamini Ronaldo tu pekee ndiye mstahili na, "wanapaswa kuwa na aibu" ikiwa watampa mchezaji mwingine tuzo ya mchezaji bora wa dunia
Pepe amedai hayo baada ya nyota huyo mwenzake wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo kuwa na msimu usio wa kawaida Ronaldo tayari amevunja rekodi kadha wa kadha ikiwemo ile ya magoli mengi ndani ya msimu mmoja wa ligi ya mabingwa ulaya
akiwa na miaka 29 sasa tayari hadi sasa ameshafunga magoli 23 ndani ya mechi 17 tu msimu huu katika michuano yote
Hata hivyo, Ronaldo anatarajiwa kukabiliana na ushindani kutoka Ujerumani kipa Manuel Neuer na nahodha wa Argentina Lionel Messi kwa Ballon d'Or,
Pepe ana wasiwasi kwamba rafiki yake tu ndiye anaestahili katika tuzo hiyo "Kwa mafanikio kama haya, wanapaswa kuwa na aibu kutokana na kile Cristiano amekuwa akifanya, kusambaratisha rekodi kibao, na kufunga mabao 17 katika Ligi ya Mabingwa msimu uliopita," "Haya mambo hayawezekani".
"Katika miezi mitatu yeye amefunga mabao 23. Nini kingine yeye ana haja ya kufanya? "Yeye ni mchezaji bora katika historia na mimi narudia. Itakuwa kashfa na aibu kama hawatampa Ballon d'Or"
Ronaldo, ambaye alishinda mwaka jana Ballon d'Or, amefunga mabao 275 katika michezo 263 tu tangu kujiunga Madrid kutoka Manchester united mwaka 2009
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni