Sports and Entertainment

Jumamosi, 6 Desemba 2014

wanawake wasisitizwa kutofumbia macho rushwa ya n gono

Hakuna maoni :
Msanii wa kizazi kipya Meninah Abdulkareem akiwa nyumbani kwake


Mwanadada wa muziki wa kizazi kipya Meninah Abdulkareem ‘Meninah,’ amewatolea uvivu ‘maprodyuza’ wanaopenda rushwa ya ngono, akisema kwake hawatafanikiwa.
Amesema anakerwa na tabia hiyo na inaweza kumfanya msanii akate  tamaa ya kufanya muziki kwa ajili ya tabia hizo.
Akizungumza juzi, Menina alisema si jambo jema kwa maprodyuza kufanya hivyo kwa sababu inawavunja moyo wasanii wachanga.
“Nasikitishwa mno na hali kama hiyo kuendelea kwenye soko la muziki na kama huwezi kumsaidia binadamu mwenzako ni bora useme kuliko kutaka rushwa ya ngono.
Meninah aliendelea kusema kamwe, hawezi kukubaliana na hali hiyo na amewashauri  wasanii wengine wa kike kupambana vikali dhidi ya jambo hilo.
“Sitakubaliana na rushwa ya ngono na wasanii wa kike tunapaswa kutolifumbia macho jambo hili,” alisisitiza Menina.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni