Bonanza

Sports and Entertainment

Jumatano, 3 Mei 2017

TAARIFA KWA UMMA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE EALA

Maoni 1 :


Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana Zanzibar katika kikao chake cha siku moja, Mei 2, mwaka huu, imewateua wafuatao kuwa wawakilishi wa CHADEMA kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA);

1. Profesa Abdalla Safari
2. Salum Mwalim
3. Ezekia Wenje
4. Josephine Lemoyan
5. Lawrence Masha
6. Pamela Massay

Walioteuliwa watakamilisha hatua zingine za uteuzi kwa mujibu wa taratibu na Kanuni za Bunge na Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki.

Imetolewa leo Jumatano Mei 3, 2017 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA


Jumamosi, 28 Machi 2015

Matumla ambonda mchina

Hakuna maoni :

Mudy Matumla akijitahidi kumbana vyema mpinzani wake
Mohamed Matumla akijitahidi kumbana vyema mpinzani wake
Bondia Mohamed Matumla amefanikiwa kutoka kimasomaso baada ya kumchapa kwa points bondia mwenzake kutoka nchini China Wang Xin Hua katika mpambano wa raundi 10 uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku.
Mpambano huo ulikuwa ni wakuwania nafasi ya kucheza katika pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa masumbwi duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr. na Manny Pacquiao unakaochezwa mapema Mei 2, mwaka huu, huko Las Vegas, Marekani.

Lewis Hamilton aongoza kufuzu Malaysia Grand Prix

Hakuna maoni :


Bingwa wa dunia Lewis Hamilton ataanza wa kwanza kwenye mashindano ya Malaysia Grand Prix
Bingwa wa dunia Lewis Hamilton ataanza wa kwanza kwenye mashindano ya Malaysia Grand Prix
Lewis Hamilton alishika nafasi ya juu kwa mara ya pili tangu aanze msimu wa 2015 kwenye mashindano ya kufudhu Malaysian Grand Prix yaliyokumbwa na mvua.
Sebastian  Vettel
Sebastian Vettel
Bingwa huyo wa dunia alimshinda nyota wa pili Ferrari Sebastian Vettel kwa sekunde 0.074 huko Sepang International Circuit.
Nico Rosberg
Nico Rosberg
Dereva mwenza wa Hamilton wa kampuni ya Mrcedes Nico Rosberg ataanza wan ne mbele ya dereva wa Red Bull Daniel Ricciardo ambaye ni wa nne.
Hali ya mvua na vimweko huko Malaysia
Hali ya mvua na vimweko huko Malaysia
MADEREVA WALIOFUDHU MBIO ZA MALAYSIA GRAND PRIX
  1. Lewis Hamilton (Mercedes) 1:49.834
  2. Sebastian Vettel (Ferrari) 1:49.908
  3. Nico Rosberg (Mercedes) 1:50.299
  4. Daniel Ricciardo (Red Bull) 1:51.541
    Daniel Ricciardo
    Daniel Ricciardo
  5. Daniil Kvyat (Red Bull) 1:51.951
  6. Max Verstappen (Toro Rosso) 1:51.981
  7. Felipe Massa (Williams) 1:52.473
  8. Romain Grosjean (Lotus) 1:52.981
    Kinda wa Toro Rosso, Max Verstappen
    Kinda wa Toro Rosso, Max Verstappen
  9. Valtteri Bottas (Williams) 1:53.179
  10. Marcus Ericsson (Sauber) 1:53.261
    Kimi Raikkonen
    Kimi Raikkonen
  1. Kimi Raikkonen (Ferrari) 1:42.173
  2. Pastor Maldonado (Lotus) 1:42.198
  3. Nico Hulkenburg (Force India) 1:43.023
  4. Sergio Perez (Force India) 1:43.469
    Jenson Button
    Jenson Button
  5. Carlos Sainz (Toro Rosso) 1:43.701
  6. Felipe Nasr (Sauber) 1:41.308
  1. Jenson Button (McLaren) 1:41.636
  2. Fernando Alonso (McLaren) 1:41.746
    Fernando Alonso
    Fernando Alonso
  3. Roberto Merhi (Marussia) 1:46.746
  4. Will Stevens (Marussia)
F1

Alhamisi, 29 Januari 2015

Apple yapata faida dola bilion 18.8

Hakuna maoni :
Simu za Iphone 6 zimekuwa zikinunuliwa sana na kuwa chachu ya faida za kampuni ya Apple
Kampuni ya kutengeza vifaa vya elektroniki, Apple, imetangaza kupata faida ya dola bilioni 18.8 katika kipindi cha miezi minne ya mwisho mwaka jana , na kuifanya kuwa kampuni ya umma iliyopata faida kubwa zaidi duniani.


Apple bila shaka imeipiku,ExxonMobil iliyopata faida ya dola bilioni 15.9 mwaka 2012 kulingana na ripoti ya kampuni ya Standard and Poor's.

Inaarifiwa hii ndio faida kubwa zaidi katika historia ya kampuni hio kuwahi kushuhudiwa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, mdadaisi mkuu wa kiuchumi wa kampuni hio, Tim Cook alisema kuwa hitaji la simu za iphone duniani ni kubwa kuindukia.

Hata hivyo, alisema kwamba hitaji la tabiti au iPad haliko juu kama ilivyotarajiwa na liliendelea kushuka kwa asilimia 18 mwaka 2014 ikifananishwa na mwaka 2013.
Kadhalika hitaji la simu ya iPhone 6 Plus lilionekana kua chachu katika faida za kampuni hio.


Hata hivyo, Apple haikufafanua mauzo ya simu ya iPhone 6 na simu nyinginezo.
Hisa za kampuni ya Apple zilipanda kwa asilimia 5 baada ya soko la hisa Marekani kufungwa Jumanne.

Mmoja wa wanaofuatilia mauzo ya bidhaa za Apple sokoni, na mhariri wa mtandao wa "Cult of Mac" aliambia BBC kwamba mauzo ya iPhone yamekuwa juu sana ikilinganishwa na matarajio.

Akosa mchumba, ajioa

Hakuna maoni :

Yasmin Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume wake atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe. 

Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40. 

Duru zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake mwenyewe katika makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na wageni wengine waalikwa.

Kwa sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio, kwani ni kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati ya watu wawili.

Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida bila ya mchumba.

Kulingana na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo, sherehe hiyo ilionekana kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani makavazi hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi zao hapo.

Aliposikia kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini alikuwa anapanga kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea mwenyewe.

"Eleby alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi na mtu mwenye nia ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr ambaye anasema harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.

Anasema anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba mtu anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.

"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.
Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani.
"ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi. ''

Orodha ya watu wenye fedha zaidi Duniani , kiasi ,umri na uraia wao

Hakuna maoni :






#1 Bill Gates $79 B             59                     United States
#2 Carlos Slim Helu & family $71.9 B
75
Mexico
#3 Warren Buffett $70.9 B
84
United States
#4 Amancio Ortega $62.6 B
78
Spain
#5 Larry Ellison $52.9 B
70
United States
#6 Christy Walton & family $41.6 B
60
United States
#7 Jim Walton $40.7 B
67
United States
#8 Charles Koch $40.4 B
79
United States
#8 David Koch $40.4 B
74
United States
#10 Liliane Bettencourt & family $40 B
92
France

VIDEO: Cristiano Ronaldo amshangaza mtoto mtaani kwa kucheza nae bila kumjua

Hakuna maoni :