Sports and Entertainment

Jumamosi, 28 Machi 2015

Matumla ambonda mchina

Hakuna maoni :

Mudy Matumla akijitahidi kumbana vyema mpinzani wake
Mohamed Matumla akijitahidi kumbana vyema mpinzani wake
Bondia Mohamed Matumla amefanikiwa kutoka kimasomaso baada ya kumchapa kwa points bondia mwenzake kutoka nchini China Wang Xin Hua katika mpambano wa raundi 10 uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku.
Mpambano huo ulikuwa ni wakuwania nafasi ya kucheza katika pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa masumbwi duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr. na Manny Pacquiao unakaochezwa mapema Mei 2, mwaka huu, huko Las Vegas, Marekani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni