Sports and Entertainment

Jumanne, 15 Julai 2014

WEMA SEPETU,,,

Hakuna maoni :

Akiwa mmoja kati ya wanadada wanofanya vizuri sana kwenye Tasnia hii ya BongoMovies ,Wema Sepetu ni msichana  anayetoka kwenye Familia ya kibalozi ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu.
Ana sura na umbo zuri sana, na mvuto mkubwa sana kutokana na rangi yake nzuri ya ngozi



 
Wema sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika hospitali ya ST. Andrew's jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia yao yenye watoto wanne wa kike.
Alipata elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha Limkokwing University. 


Wema alianza kuigiza rasmi mwaka 2007 alipoonekana kwenye filamu ya POINT OF NO RETURN ambapo halicheza kama mke wa jamaa tajiri mchawi ambaye daima huua wapenzi wake wa kike kama sadaka. Wema alifikiri angeweza kufa pia lakini aliamua kumwomba Mungu na mwishowe alifanikiwa kuiokoa familia yake na yeye.
Pamoja na filamu hizi Wema ameigiza kwenye filamu nyingine nyingi kama Red Valentine, White Maria, Tafrani, Sakata, Crazy Tenant, Diary, Lerato, Dj Benny and Basilisa zilizompatia umaarufu na mafanikio makubwa.
Pamoja na kuwa na kipaji cha uigizaji wema pia anakipaji kikubwa cha kuimba na pia alishawahi kushiriki mashindano ya urembo na kufanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania mnamo mwaka 2006 na kujipatia zawadi ya gari aina ya Toyota Rav 4

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni