Sports and Entertainment

Jumatano, 11 Juni 2014

Magazeti huko maajuu

Hakuna maoni :
Arsenal huenda wakamkosa kipa wa  Real Madrid Iker Cassilas baada ya mpenzi wake kudai kuwa hatohama kutoka mji mkuu wa Spain, Madrid (Daily Express),lakini Arsenal huenda wakamsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata na wapo tayari kupambana na Tottenham na Inter Milan wanaomtaka pia (Daily Express), Barcelona wamefikia makubaliano yasiyo rasmi na Marcus Reus wa Borussia Dortmund. Reus amekuwa akifuatiliwa pia na Manchester United (Talksport), wakati huohuo Manchester United wapo tayari kupokea pauni milioni 12 kwa kiungo wake Marouanne Fellaini ambaye alisaini mwaka jana kutoka Everton kwa pauni milioni 27 (Daily Star), Chelsea wanajaribu kumsajili Cesc Fabregas kutoka Barcelona katika mkataba ambao utahakikisha Arsenal haipati nusu ya faida itakayopata Barcelona (Daily Telegraph), Pepe Reina atarejea Liverpool kwa kuwa Napoli inashindwa kufikia madai ya Liverpool ya kubadili mkataba wa mkopo kuwa wa moja kwa moja (Metro), Manchester City watakamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Porto, Fernando ifikapo mwisho wa wiki hii na pia kukamilisha usajili wa Bacary Sagna kutoka Arsenal(Daily Mail), Everton wana tumaini watafanikiwa kupambana na Arsenal katika kumsajili Samuel Eto'o kutoka Chelsea (Daily Express)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni