Sports and Entertainment

Ijumaa, 27 Juni 2014

Diego Maradona : mtupeni Suarez Guantanamo

Hakuna maoni :

Suarez akishika meno yake kuangalia yapo aua yametoka naada ya kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini wakati Uruguay ilivyomenyana na Italia kweny mashindano ya Kombe la Dunia 2014, Brazil.
Suarez akishika meno yake kuangalia yapo auyametoka baada ya kumng’ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini wakati Uruguay ilipokuwa inamenyana na Italia kwenye mashindano ya Kombe la Dunia 2014, Brazil.
Diego Maradona ameponda adhabu ya Fifa dhidi ya mshambuliaji Luis Suarez aliyemuita mhalifu na kusema shirikisho hilo la soka la kimataifa lilipaswa kumtia pingu na kumfunga kwenye gereza la Guantanamo.
“Nani alimfanya Suarez auwe?,” Maradona aliyasema hayo wakati wa kipindi cha kutoa maoni cha Venezuela Telesur na televisheni ya serikali ya Argentina siku ya Alhamisi usiku.
“Hili ni soka, huu ni mkataba,”alisema gwiji huyo wa Argentina. “Wangeweza hata kumtia pingu na kumpeleka Guantanamo moja kwa moja.”
Guantanamo ni gereza lenye utata la Marekani lililopo nchini Cuba, lilifunguliwa wakati wa utawala wa Bush, linakosolewa zaidi na makundi ya haki za binadamu kwa kuwafunga watu kwa vipindi visivyojulikana bila mashtaka wala kesi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni