Ijumaa, 20 Juni 2014
Duh!!! Hafsa Kazinja aukimbia Uislamu,,, kisa ; mashetani kumuandama
Mwanamuziki Hafsa Kazinja anayetamba na Wimbo wa Mlala Nje huku video yake ikiwa tayari, ameamua kuikacha dini yake ya Kiislam na kuhamia kwenye Ukristo. Hafsa alisema alifikia uamuzi huo baada ya kusumbuliwa na maruhani ambayo yalimfanya arukwe na akili.
“Niliumwa sana hadi ikaonekana nimerukwa na akili, maruhani ndiyo yaliyokuwa yananisumbua. Kuna kipindi yalikuwa yakiniambia nisile samaki wala dagaa, mara yakaniambia natakiwa kuwa mganga.
“Njia zote ziligonga mwamba, nikaambiwa nisali na nimuachie Mungu, nikawa nikisali sauti zinanijia nimtukane Mungu tena matusi makubwa, nimeenda hadi kwa waganga, mashehe na walokole wakaniombea na nikapoteza pesa nyingi hadi nikauza nyumba yangu na magari lakini wapi. Nimekwenda Kanisa la Zoe ndiyo nimepona, namshukuru Mungu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni