Sports and Entertainment

Jumatatu, 16 Juni 2014

Eto'o mguu ndani mguu nje kwa Croatia

Hakuna maoni :
Nahodha wa cameroon, Samuel Eto'o anatazamiwa kukosa mechi dhidi  ya Croatia siku ya Jumatano kutokana na majeraha.
Eto’o hajafanya mazoezi kwa siku mbili na huenda asipone kwa wakati kwa ajili ya mechi muhimu ya Kundi A mjini Manaus.
Mshambuliaji huyo, 33, aliandika kwenye Twitter; “Madaktari wamethibitisha kuwa sitoweza kucheza kwa sababu ya majeraha ya goti yanayonisababishia maumivu”
Cameroon na Croatia wote walipoteza mechi zao za ufunguzi na wanakabiliwa kutoka kwenye mashindano.
Simba hao wasiofugika walifungwa goli 1-0 na Mexico, huku Croatia wakiambulia kichapo cha magoli 3-1 kutoka kwa wenyeji wa mashindano Brazil.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni