Rais wa shirikisho la soka nchini Ghana , amekanusha madai kuwa shirikisho hilo lilikubali timu ya Taifa kucheza katika mechi ambazo timu nyingine zilikuwa zinajiandaa kupanga.
Shirikisho hilo, pia limewataka polisi kuchunguza madai hayo. "madai yaliyotolewa na gazeti hilo sio ya kweli,'' alisema Rais wa shirikisho la soka la Ghana GFA Kwesi Nyantakyi.Madai yenyewe yalitolewa kufuatia uchunguzi uliofanywa na wandishi wa jarida la The Daily Telegraph.
Shirikisho hilo limewataka maafisa wa polisi kuchunguza madai ya vyombo vya habari vya Uingereza kwamba mmoja wa maafisa wake alikubali timu ya nchi hiyo kucheza katika mechi zilizo fanyiwa ufisadi.
Nyantakyi aliambia BBC kuwa ana waraka wa kurasa saba kujibu madai hayo na pia anatafakari kuichukulia hatua za kisheria jarida hilo na kitio kilichotoa harai hizo z auongo.
Uchunguzi huo ulisema kuwa watu wawili mmoja ambaye ni wakala wa FIFA na mwingine afisa wa soka nchini Ghana ambao walisema kuwa na uwezo wa kupanga mechi, wangeweza kupanga mechi nyepesi za kirafiki ambazo zingehusisha timu ya Ghana ambao wanacheza katika kombe la dunia.
Madai hayo hata hivyo hayahusishi michuano inayoendelea nchini Brazil
Ripoti hiyo ilisema kuwa bwana Nyantakyi alikubali Ghana kucheza michuano miwili baada ya kushiriki kombe la dunia.
"Sijawahi kukubali kupanga mechi inayohusisha shirikisho la soka Ghana.''
"Nipokea mkataba kutoka kwa wakala wa FIFA ambao mimi sijasoma na kwa hivyo kusema kuwa niliukubali sio sawa,'' alisema bwana Nyantikye.
Mamlaka ya Soka nchini Ghana imekana madai ya jaribio lolote la kuuza mechi zake ama kuhusika kwa afisa yeyote katika ufisadi.
Madai hayo yametolewa kufuatia uchunguzi wa pamoja kati ya gazeti la Uingereza la Daily Telegraph na Runinga ya Channel Four.
Katika taarifa yake shirikisho la soka duniani FIFA limesema kuwa hakuna ushahidi kwamba uadilifu wa michuano ya kombe la dunia umeathirika.
Shirikisho hilo limesema kuwa litamuwekea vikwazo vikali afisa yeyote atakayepatikana na makosa hayo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni