Sports and Entertainment

Alhamisi, 26 Juni 2014

Herrera akutana na maafisa wa Manchester United

Hakuna maoni :

Ander Herrera anakutana na maafisa wa Manchster United uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo Carrington akiwa mbioni kuhamia Old Trafford.
Kiungo huyo wa Athletic Bilbao alikutanishwa na Sir Bobby Charlton na kupokelewa kwa sherehe mjini Carrington baada ya kuwasili na VW transporter nyeupe kabla ya kuonyeshwa mazingira, akiwa pamoja na wakala wake.
Daktari wa klabu alikuwepo, japo vipimo vya afya bado kwa kiungo huyo aliyegharimu uhamisho wa yuro milioni 35, huku Mashetani wekundu wakitaka kumaliza biashara mapema kabla dau halijapanda na kufikia yuro milioni 40 ifikapo Julai 1.
Herrera atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Louis van Gaal.
Aliwaaga mashabiki wa timu yake ya Athletic Bilbao kabla hajaondoka Hispania, United wameahidi kumlipa kitita cha yuro 180,000 kwa wiki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni