Jumatano, 18 Juni 2014
Japan wafungia picha za Ngono
Japan imefungia umiliki wa picha za mapenzi za watoto, ikiwa ni moja ya nchi zilizoendelea kufanya hivyo.
Sheria hiyo mpya inaeleza kwamba yeyote atakayeonekana na picha za matusi za watoto atafungwa jela mwaka mmoja au kupigwa faini ya dola 10,000 (mil. 17 za kitanzania).
Sheria hiyo haitumiki kwa picha za sanaa za wanyama au za kuchekesha zinazojulikana kama manga.
Hapo awali Japan ilikuwa kwenye Muungano wa 34 wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo uliokuwa hauna maonyesho hayo.
Wachambuzi wanasema kuna pingamizi kubwa kutoka kwa wasanii wa manga, watoa maoni na wachapishaji.
Wanasema itazuia utoaji huru wa mawazo na kufanya uongozi kufanya maamuzi ya upatanishi kuhusu sanaa.
Chama cha Wachapishaji wa Majarida Japan, ambacho huwakilisha asilimia 90 ya makampuni ya uchapishaji, kilituma taarifa kwenye mtandao wake mwezi Juni kuwa sheria hiyo inaleta maumivu dhidi ya wasanii na utamaduni wa kuchapisha.
Mwandishi wa BBC Rupert Wingfield-Hayes aliyeko mjini Tokyo anasema Japan bado inachukuliwa kama moja ya vituo duniani vinavyotumia na kubadilisha picha za matusi za watoto.
Uhalifu unaohusisha ponografia za watoto umeripotiwa kuongezeka nchini Japan.
Tanzania je?, hivi serikali inafahamu kuwa ukizunguka katika mitaa ya miji kama Dar Es Salaam, Tanga, Arusha, Mbeya na hata Moshi utakuta vibanda vya kuonyesha sinema za ngono huku vikiwa vimejazwa na watoto wa shule za msingi na sekondari, wakati mwingine hadi watu wazima? Serikali inajua?mnalichukuliaje?
Picha hizo huitwa ‘pilau’, maadili yanazidi kuporomoka katika jamii ya kitanzania, picha hizo huuzwa wazi wazi nchini.
Zinaingiaje?
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni