Sports and Entertainment

Alhamisi, 19 Juni 2014

Kim Amzawadia Kanye sh.32,000 siku yake ya kuzaliwa

Hakuna maoni :

Kim Kardashian akiwa katika moja ya maduka ya Boutique jijini New York.
Kim Kardashian akiwa katika moja ya maduka ya Boutique jijini New York.
Ni mtu ambaye ana kila kitu kizuri anachotaka- – mamilioni ya dola, familia nzuri, maisha ya muziki ambao yanazidi kufanikiwa zaidi.
Hivyo kumchagulia zawadi sahihi Kanye West wala hakuhusu kiasi cha pesa wala mawazo mengi, hivyo ndivyo alivyofanya mke wake Kim Kardashian kwa rapa huyo, 37.
Mrembo huyo 33, ambaye alifunga ndoa na mumewe mwezi uliopita mjini Florence, Italia, alimpa Kanye kidude cha mchezo ambacho kilimgharimu dola zisipongua 20 (sh. 32,000).
Nyota huyo wa mchezo wa runinga alimnunulia mumewe kifaa hicho kinachoitwa Monopoly, ambacho kinamruhusu mnunuaji kutaka bidhaa, kutengeneza kadi na kubuni michezo mbalimbali, kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa Juni 8.
Kweli mapenzi ya kweli hayapimwi kwa kupeana zawadi zinazogharimu fedha nyingi, mapenzi ya kweli hupimwa kwa thamani ya moyo wa kila mwenza ambao haulinganishwi na chochote duniani kiwe ardhini au baharini.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni