Ijumaa, 20 Juni 2014
Lupita Nyong'o apamba ukurasa wa jarida la vogue
Kim Kardashian ndiyo nani? Inaonekana kama 2014 umekuwa mwaka wa Lupita Nyong’o!
Ni miezi kadhaa tu imepita tangu achukue tuzo ya Oscar kama mwigizaji wa kike msaidizi kwa kufanya vizuri kwenye filamu ya 12 Years a Slave, nyota huyo wa Hollywood ametokezea kwenye ukarasa wa mbele wa jarida la Vogue.
Akiwa amevalia gauni, nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, mzaliwa wa Kenya anaonekana kutokuchoka baada ya kutolewa Julai kwenye mitindo ya Biblia.
Akiwa kwenye mahojiano,Nyong’o alizungumzia kuhusu umaarufu na kudai kuwa hajihisi kuchanganyikiwa anapokuwa kwenye umma unaomzunguka.
“Inaonekana kama tasnia ya burudani imevamia katika maisha yangu”, alisema Lupita.
“Watu walioonekana kuwa mbali na mimi ghafla nawaona mbele yangu na kudai kunijua – kabla ya mimi kuwajua”.
“Hata kwenye ndoto zangu za kuwa muigizaji, ndoto yangu haikuwa umaarufu. Ndoto yangu ilikuwa ni kufanya nilichotaka kufanya”.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni