Jumatano, 18 Juni 2014
Mwili wa mtu wasitisha shughuli za Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta
Shughuli zimerejea teana kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta baada ya barabara ya ndege kufungwa kwa dakika 40 mapema leo Jumatano, taarifa hiyo imetolewa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya.
Maafisa wa usalama waliifunga barabara hiyo kwa muda mfupi baada ya kuonekana kwa mwili wa binadamu kwenye ukingo wa barabara hiyo majira ya saa 12 asubuhi.
Polisi wanasema bado hawajajua mwili wa mwanaume huyo ulifikaje na kuongeza kuwa wanashuku kuwa huenda mtu huyo alijificha kwenye sehemu ya matairi ya ndege.
Maafisa hao wamesema waliitwa kwenye majira ya saa 12 asubuhi na kuarifiwa kuwa kuna mwili mwishoni mwa barabara kuu ya ndege na kwenda kutazama wakakuta mwili huo na michubuko. Mkuu wa Uwanja wa ndege Joseph Ngisa amethibitisha kuwa mwili huo ulikuwa na michubuko wakati ulipoonekana.
“Hatujui kuwa kama alikuwa amejificha au ni mtu alikuja mwenyewe kwenye barabara ya ndege”, alisema Ngisa.
Alisema mwili huo haukuwa na taarifa za utambulisho.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni