Alhamisi, 19 Juni 2014
Orodha ya Watangulizi wa Kanye West katika Penzi la Kim
Vitu ambavyo watu wanavifanya chumani ni siri yako na mwezi wako lakini mara nyingi unapokua maarufu basi vitu hivi sio siri tena.Hivi sasa kim ameshaolewa na bwana Kanye lakini mikasa aliyoipata katika maisha yake ya mapenzi ndio imetufanyavibe Tanzania kuangalia kwa jicho la pili mahusiano aliyopitia bibie Kim Kardashian.Akiwa tayari ana miaka 31 , Kim amepitiwa na wanaume wengi huku wengine wakiwa ni mpango wa kando wakati tayari ana mtu mwingine. Hii ni list ya wanaume (wanaojulikana na maarufu)ambao wameshawai kumpitia kim tokea mwaka 1994 :-
TJ Jackson (1994-1998)
katika interview yake na Oprah, Kim alisema alianza kutumia njia za uzazi akiwa na miaka 14 ambapo alikua ataki kushika mimba akiwa na mdogo. TJ Jackson kama ulikua hujui, huyu ni mpwa “nephew” wa Michael Jackson ambapo inasemekana ndio alikua sio tu wa kwanza kutoka naye bali wa kwanza pia kufanya naye mapenzi.
Damon Thomas (2000-2004)
Unafikiri kim hakuwahi kuolewa kabla? basi kama ndio , habari ni kwamba kim akiwa na umri wa miaka 20 aliolewa na producer , Damon Thomas , ndoa iliyodumu kwa miaka minne tokea mwaka 2000 hadi mwaka 2004. Ndoa yao ilivunjika kutokana na kim kupigwa mingumi na mwanaume huyu . Pia Kim alikua akifuatiliwa kila dakika anapopumua.
Julian St. Jox (2001)
Huyu Jamaa ambaye ni muigizaji wa muvi za kikubwa (pornstar) ambaye alimmaliza kim wakati kim akiwa yupo kwenye ndoa katika party moja waliokua nae. Julian alisema kim alitokea katika hoteli ya Wyndham na mwanaume mweusi ambae anahisi alikua mme wake kipindi hicho, Damon ambapo alimfuata kim huku akiwa na pornstar mwenzake wa kike Emily Ann ambapo walianza kucheza na mizuka kupanda ambapo watatu hao walitafuta chumba na mengine yakabaki kua story.
Ray J (2002 – 2003)
Hivi kunaaja ya kuielezea hii kitu ? kwa wale wanaopenda picha za ngono , mtakua mmeshaona mkanda wa ngono kati ya Ray J na Kim Kardashian uliovuja. Kipindi mkanda huo unarekodiwa , Kim Kardashian alikua bado yupo kwenye ndoa yake na Damon. Duh! jamaa alikua bwege kweli…Kumbuka mkanda huu wa ngono ulivuja mwaka 2007 japokua ulirekodiwa mwaka 2003. Kama ulikua hujui mwaka 2007 ndio ulikua mwanzo wa kipindi cha Keeping up with the kardashians na wataalamu wanasema kipindi hiki kililenga kumsafisha kim bila kujua mafanikio ambayo kingepata.
Nick Lachey (2006)
Mwanamuziki huyu kutoka bendi ya 98 Degrees alitoka na Kim Kardashian kwa wiki moja tu na mahusiano yake yakavunjika. Nick alikua ametoka kuvunja ndoa yake na mwanamuziki Jessica Simpson na muda mchache akaanza kutoka na kim. Nick anadai Kim alimtumia kujipatia umaarafu baada ya kusema kim aliwalipa mapaparazi zaidi ya 30 kumpiga picha walipokua wanatoka movies. Nick anasema picha zake kati yake na Kim ndio ulikua mwanzo wa mafanikio ya Kim.
Nick Cannon (September 2006- January 2007)
Hehehe, unajua kwanini Nick Cannon alimtosa Kim kardashian ? wapenzi hawa walikua wakiishi vizuri hadi pale Kim alipoulizwa na Nick kuhusu kuwepo kwa mkanda wa ngono kati yake na Ray J na Kim kumdanganya na kumwambia hamna kitu kama hicho. Nick alisema hataweza kumsamehe Kim kwa uwongo aliyomwambia.
Reggie Bush (2007)
Huyu ni mchezaji wa mpira (NFL) wa marekani ambae alikua na mahusiano na kim kwa zaidi ya miaka miwili hadi mwaka 2009 lakini mahusiano yao yalikua yakutosana na kurudiana baadae.
Evan Ross (2007)
Huyu ni mtoto wa mwanamuziki wa zamani na maarufu kabisa nchini marekani, Diana Ross. Wawili hawa walitoka pamoja kipindi kardashian alipuamua kupumzisha penzi la Reggie Bush.
Christiano Ronaldo (April 2010)
Hiki kipindi mrembo Kim alikua nchini Hispania kimapumziko ndipo alipokutana na Christiano Ronaldo. Kipindi hicho christiano akiwa na miaka 25 huku Kim akiwa na 29 , wawili hao walionekana kwa mara ya kwanza wakipeana mahaba ndani ya siku 3 ambazo kim alikua nchini humo.
Shengo Deane (April 2010)
katika interview yake ya Piers Morgan kim alieleza jinsi alivyohuzunika kuhusu sex tape yake ya mwaka 2007 lakini chaushangaza aliweza kuonyesha mahaba yake na Shengo Deane katika kipindi cha keeping up with the Kardshians. Kumbuka mu-Australia huyu alikua ni bodyguard wa Kim Kardashian.
Miles Austin (June 2010)
Huyu naye ni mchezaji wa American Football. Wawili haya walidumu kwa miezi na hakuna sababu ya msingi ya kutengana kwao zaidi ya long distance.
Michael Copon (October 2010)
huyu ni muigizaji aliyemjua Kim kwa zaidi ya miaka 11 na baadae wakafanya yao japokua uhusiano wao haukudumu kabisa kwa alichokisema Michael kwamba Kim anatabia za kitoto.
John Mayer (October 2010)
Hii ilikua mwishoni mwa mwezi October ambapo kim aliamua isiwe tabu na kumuachia mwanamuziki na producer , John Mayer ale mema ya nchi
Gabriel Aubrey (November 2010)
Huyu ni model kutoka nchini Canada na kipindi anatoka na Kardashian alikua ana mtoto wa miaka miwili aliyezaa na msanii Halley Berry.
Kris Humphries (2010-2013)
Hii ilikua ndoa ya pili kwa kim Kardashian. Hii ndoa kati ya Kris Humphries na Kim Kardashian ni maarufu kwasababu iliweza kudumu kwa siku 72 tu ! Ndoa ya mcheza kikapu huyu wa NBA na Kim ilifika mwisho baada ya Kim kuhisi kwamba hamna jema litakalotokea baadae na Kris pia kuhisi Kim anachepuka kwa rapper Kanye West.
Kanye West (2007 hadi leo)
Unashangaa nini sasa ? Kim Kardashian alikua akichepuka kwa Kanye kipindi ana mahusiano na Reggie Bush na Kris Humpries.Kwasasa Kim na Kanye ni wanandoa na wanamtot mmoja, North West.
Duh, hivi kwa hii list wewe ungekubali kumuoa Kim kwa mara ya tatu kama alivyofanya kanye tena ukizingatia kuna wengine waliopita sema bila uhakika kama 50cent, The Game, Brett Lockett, Scot Storch na wenine wasio celebrities ?
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni