Jumatano, 18 Juni 2014
Pat Patterson ; Mimi ni Shoga
Nguli wa mchezo wa mileleka katika WWE, Pat Patterson, ametangaza rasmi baada ya siri iliyodumu kwa muda wa miaka 50, bila kuweka wazi kamba yey ni mshiriki wa mapenzi ya jinsia moja
mwanamieleka huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 73 sasa aliyasema hayo katika mtandao wa WWE kupitia kipindi cha legends' house alisema"kwa mara ya kwanza katika maisha yangu , mimi ninakuwa mimi"
taarifa zinasema kwamba Pat , ambaye ameishi maisha hayo ya kujificha kwa zaidi ya miongo mitano sasa alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mshirika wake ambaye sasa amefariki dunia kutokana na matatizo ya moyo.
Pat amekuwa karibu na mkurugenzi wa WWE vince McMahon kwa karibu miaka kumi sasa, pia ndiye kuwa bingwa wa kwanza wa kimataifa wa kampuni hiyo na alisaidia utengenezwajiwa michuano ya royal rumble
baada ya kujitangaza rasmi tamko la nyota huyo lilipokelewa kwa hisia na msisimko mkubwa huku baadhi ya mastaa wa mchezo huo wakisema kwa sauti "Pat tunakupenda,,,,hakika tunakupenda na kila siku itabaki hivyo"
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni