Jumanne, 24 Juni 2014
Raisi kikwete atoa tamko kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
Rais JAKAYA KIKWETE ameitaka ofisi ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kuanza kujifunza ili kuwa na uelewa wa namna ya kukagua makampuni ya gesi yaliyopo hapa nchini
Rais JAKAYA KIKWETE ameitaka ofisi ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kuanza kujifunza ili kuwa na uelewa wa namna ya kukagua makampuni ya gesi yaliyopo hapa nchini kutoka kwenye nchi zenye uzoefu na kazi hiyo na siyo wasubiri mpaka gesi ianze kuchimbwa ndipo waanze kulalamika.
Rais KIKWETE ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali unaohusisha nchi zaidi ya KUMI na NANE.
Rais KIKWETE ameitaka ofisi ya CAG isipoteze uaminifu na imani waliyonayo wananchi juu yake badala yake iongeze juhudi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Rais KIKWETE pia ameutumia mkutano huo kuzindua kitabu maalumu ambacho ni muongozo kwa wakaguzi kinachoitwa: Transformation of National Audit Office of TANZANIA.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni: kuimarisha Uhuru wa ofisi kuu za Taifa za ukaguzi ili kuwezesha uwajibikaji utakaopelekea ukuaji wa uchumi
.

Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni