Sports and Entertainment

Jumatano, 18 Juni 2014

Raisi yupi anapendwa zaidi Marekani?

Hakuna maoni :

Rais wa 42 wa Marekani ndiye anayehusudiwa zaidi kuliko rais mwengine kwa miaka 25 iliyopita. Inasemekana kuwa watu weusi walikuwa wakimuita Black President.
Bill Clinton alikuwa Rais wa 42 wa Marekani, ndiye anayehusudiwa zaidi kuliko rais mwengine kwa miaka 25 iliyopita. Inasemekana kuwa watu weusi walikuwa wakimuita Black President.
Ni Rais yupi wa Marekani ambaye anapendwa zaidi kwa miaka 25 iliyopita?
Kutokana na utafiti mpya uliofanywa na Wall Street Journal, NBC News na Anneberg, umedai kuwa rais huyo ni Bill Clinton.
Walipoulizwa kuwa ni rais yupi wa Marekani wanaomhusudu, asilimia 42 walimtaja rais huyo wa 42 – akiwa na zaidi ya mara mbili asilimia kwa marais wengine.
Wengine walipata asilimia sawa kutoka kwa wananchi: Rais Barack Obama (asilimia 18)
, Rais George W. Bush (asilimia 17)
 na Rais George H.W. Bush (asilimia 16).
Kura za watu 1,238 za watu wazima zilichukuliwa kuanzia Juni 2-8, karibia wiki kabla ya Mzee Bush hajateka vichwa habari kwa kushereheka miaka 90 ya kuzaliwa kwa kuruka kutoka kwenye ndege.
Kupendwa kwa Bil Clinton kwa mujibu wa wapiga kura ni kwamba ni “namna alivyofanya kusafisha wasifu wake” tangu aondoke White House 2001.
Ila Clinton, amefanya kazi kubwa ya hisani kupitia wakfu wake ya Bill Clinton Initiative, ila alishakuwa akihusudiwa na wengi tangu aondoke White House.
Ila kutokana na utafiti wa Gallup uliofanywa mapema June, ilithibitika kuwa Rais Obama ana asilimia 44.
Tanzania nayo haina budi kufanya utafiti na kujua ni Rais gani anahusudiwa zaidi tangu Mwalimu Nyerere alipomuachia ofisi Al Haj Ali Hassan Mwinyi, ambapo ni miaka 29 iliyopita.
Maana wa sasa anavyoandikwa, inabidi utafiti huu ufanyike tukate mzizi wa fitina…

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni