Sports and Entertainment

Jumamosi, 28 Juni 2014

SUAREZ: KICHWA CHA MWENDAWAZIMU NA MIGUU MITAKATIFU

Hakuna maoni :


Suarez, Suarez, Suarez kama ingekuwa Ni nyimbo kwa wenzetu kwa Raisi Obama wangesema ipo chart za juu kabisa katika Billboard. Bahati mbaya haipo hivyo, kwa wakati huu ni mchezaji na vimbwanga vyake. Kwa sasa yupo jela ya soka, jela kweli kweli. Hatouona uwanja kwa miezi minne, hatokuwa na siti yake pale uwanja wa anfield kwa mechi zaidi ya tisa. Bahati mbaya sijamsikia akisema chochote. Kawa mjanja huyu, anajua kwa kauli yoyote itadadavuliwa sasa kaacha mapambano Kati ya watetezi na walalamikaji, Ni kama tamthiliya machoni lakini Ni,uhalisia.

Mara nyingine soka huwahitaji watu hawa, media zinawapenda sana watu hawa. Unamfahamu Paul Gascoigne maarufu kama Gazza. Inawezekana hajazaliwa mchezaji kipaji kama huyu mtu, lakini Lady Gaga wa Marekani hakufikia nusu ya visanga vyake, Erick Cantona aliwahi kupiga Kung Fu shabiki na bado aliporudi akafunga goli Kisha akageuka mithili ya mtume anaeutizama Ulimwengu aupatie baraka zake. Hata Suarez alifungiwa mechi 11 Kisha akarudi akafunga goli 31 na,msaada Mara 12 katika mechi 33. Hivi ndivyo wachezaji wazuri walivyo. Unamtukana kwa ulevi kama Gaza anarudi anapiga tobo watu watatu Kisha anapiga pasi ya mwisho tamu mithili ya cake ya maharusi. Anapiga teke shabiki mnamtukana Kisha anafunga goli la ajabu anawageukia mnampigia makofi zaidi ya alopigiwa mheshimiwa Jakaya siku ya kuapishwa Uraisi. Mwisho mnataka auzwe kwa kukosa mechi 11 anarudi nafunga magoli, anavunja rekodi Kisha mnaliimba jina lake kwa ustadi uliotukuka, mnaamini ndio alie bora, mnamlilia, mnampigia kura Kisha mnafungua vizibo vya vinywaji vyenu kwa furaha ya magoli yake.

Wakati sehemu kubwa ya ulimwengu ikiamini Suarez haufai mchezo wa soka, wakati sehemu kubwa ya ulimwengu ikimwona Ballotelli malaika mbele ya Suarez, kwao Uruguay ni tofauti, wao ni Mungu mtu, wao wanaamini Suarez alikuwa na maana yake, wakati anadaka mpira pale kwa Madiba Kisha Ghana anatoka, Kisha akawafunga waingereza kwa miguu iliyokuwa na nyuzi za mshono, wao wanaamini huyu ndo shujaa wao, wanatamani Hata goli la Godin dhidi ya Italy lilitokana na uhuni wa Suarez. Wanaamini ile iliwatoa Italy mchezoni na dakika mbili baadae wakafungwa. Sio ajabu ndo maana Hata baada ya adhabu walijaa airpot kumpokea kama Watanzania tulivyojaa katika barabara alizopitia Mheshimiwa Barack Obama. Wakati Van Persie akiumizwa na majeraha yake yanayomweka nje tangu anacheza soka la kiwango cha juu, kwa Suarez ni tofauti, Mungu kamjalia mifupa migumu na roho ngumu lakini ni ajabu tangu mwaka 2011 pasipo kupewa kadi nyekundu amekosa michezo 34 kwa adhabu.

Nawaza Tu ningepewa bahati ya kukutana na Nelson Mandela huko alipo angenambia nini kuhusu huyu mtu, naamini Hata yeye aliamini kwa sasa atakuwa ameacha, natamani yule dereva wa magari ya mbio ndefu Michael Schumacher akipona akaambiwa habari za Suarez atasema nini, maana wakati anapata ajali Suarez alishawafunga Norwich goli 4 peke yake. Lakini pamoja na yote anajiamini, usishangae akarudi October akawa mfungaji bora tena, akawa mkombozi tena, akayafuta machozi ya mashabiki wanaoweza kuwa wamekata tamaa, akarudisha Mbwembwe za Mbwiga Mbwiguke nasikia ni shabiki wa kutupwa wa Liverpool. Hii ndo raha ya kuwa fundi. Nasikia mashabiki wa Liverpool wanataka auzwe, hatari kweli, anauzwa Kisha unamleta nani? Nyakati zimebadilika, hiki sio,kipindi ambacho Owen alikuwa Liverpool De lima alikuwa Madrid, Nisterlooy alikuwa Man U, Henry alikuwa Arsenal. Na Drogba alikuwa ligi ya Ufaransa. Mchezaji wa uwezo wa Suarez kumpata ni ngumu, kupata magoli 31 na assist 12 ni ngumu. Najua Suarez alipo anacheka, najua anawaonea huruma, anajiuliza akipishana na Sanchez anapungukiwa nini, anawaza,akienda Madrid anashindwa nini na mwisho anawaza akibaki Liverpool atashindwa na nani. Baada ya hapo anajiona bingwa, anajiona kamanda haswa, pamoja na uhuni bado atahitajika, bado atanunuliwa kwa gharama ya Bale. Ni mkombozi huyu japo mhuni. Atachukiwa kwa muda mfupi baadae ataliliwa kwa furaha Ana uhakika huo. Ndo maana si ajabu akijengewa Nyumba ya kifahari pale pembeni mwa uwanja wa ndege Montevideo Uruguay, naamini kila mwanauruguay ataliunga mkono ili, Hata wakitolewa na Colombia hawataumia san watajitetea Mkombozi wao hakuwepo, usiwalaumu, wao hawaamini katika kichwa chake wanaipenda kazi ya miguu yake, ndo maana hata wakienda kumpokea hawatashika kichwa watainama na kumbusu miguu. Hawajali kama Ana kichwa cha mwendawazimu wanachoamini Ana miguu ya kitakatifu. Ahsanteni
By Nicasius Coutinho Suso

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni