Sports and Entertainment

Jumamosi, 21 Juni 2014

vichapo ilvyotoa COSTA RICA ,,,, FIFA kuichunguza juu ya dawa za kuongeza nguvu

Hakuna maoni :

Kila mechi, FIFA huchukua wachezaji wawili kutoka kila timu kwenda kufanyiwa vipimo vya dawa za kuongeza nguvu.
Wakati Costa Rica wakiishangaza dunia kwa kuifunga Italia 1-0, FIFA waliwaita wachezaji saba wa Los Ticos kwa ajili ya vipimo vya dawa za nguvu, kiliripoti chombo cha habari cha Italia.
Fifa waliamua kufanya hivyo baada kuahirisha kufanya zoezi hilo kipindi cha nyuma.
Hilo limeonekana kama tatizo kidogo.
Kipigo cha Italia kimewashtua FIFA na kuamua kuwaita zaidi ya mara tatu kiasi wachezaji hao kwa kuwachunguza kama walitumia madawa.
Pamoja na maelezo hayo ya FIFA, wachezaji wa Costa Rica hawakufurahishwa.
Mlinda mlango Keylor Navas alisema, “Tulikereka kidogo,”
Ruiz alisema, “Ila hatuna jinsi. Hakuna cha kuficha. Tumejiandaa vya kutosha, bila kutumia vitu vilivyokatazwa. Nafikiri, ni asili ya binadamu kutoamini kile tunachokifanya”.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni