Jumanne, 24 Juni 2014
waandishi saba wa aljazeera wawekwa kifungoni Misri
Waandishi wa habari watatu wa shirika la habari la al-Jazeera wanaotuhumiwa kuunga mkono kundi la Muslim Brotherhood wamefungwa miaka saba jela nchini MIsri.
Mahakama mjini Cairo imemkuta na hatia Peter Greste, Mohamed Fahmy na Baher Mohamed kwa kusambaza habari za uongo na kuunga mkono kundi ambalo sasa limepigwa marufuku.
Watatu hao walikanusha mashtaka hayo.
Washtakiwa wengine 11 walihukumiwa bila ya kuwepo mahakamani, wakiwemo waandishi watatu wa habari wa kimataifa, kifungo cha miaka 10 jela.
Kesi hii imeleta shutuma nyingi kimataifa kwa madai kuwa imehusishwa na sababu za kisiasa.
Peter Greste (pichani) aliwahi pia kuwa mwandishi wa BBC.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni