Jumatano, 30 Julai 2014
Diva aanika mapaja yake hadharani na aonyesha dole la kati
Mtangazaji wa kipindi cha mahaba kiitwacho Ala za Roho kupitia Radio Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ hivi karibuni alilazimika kuyaanika maungo yake ya sehemu za mapaja kushuka chini baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mmoja wa mashabiki wake.Kupitia blog yake, Diva alidai kuwa siku za nyuma kuna mtu aliomba kuona sehemu hizo za mwili wake hivyo baada ya kumbania sana ameamua kumtimizia haja yake ili afurahi.
“Kuna mtu alikuwa akidai hajawahi kuona miguu yangu iko ikoje na kwamba nimekuwa nikionesha sehemu ya shingo tena kwa upande,leo nimeamua kumfurahisha,”alisema Diva. Sambamba na maneno hayo, mtangazaji huyo alijifotoa picha zilizoocha wazi sehemu kubwa ya mapaja yake kisha kuziweka kwenye ukurasa huo.
Diva ni mtangazaji mwenye sauti ya kimahaba, yenye uwezo wa kumtoa nyoka pangoni ambaye watu wengi wamekuwa na hamu ya kumuona jinsi alivyo kwani wamezoea kumsikia redioni tu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni