Dudubaya anajulikana kama mmoja wa Wasanii wa siku nyingi bongoflevani ambae pamoja na headlines zake binafsi huwa anasikika mara chache akizungumzia au kutoa ushauri kwa ishu kadhaa za Wasanii wenzake.
Baada ya kusikia yanayoendelea kati ya mastaa wa bongofleva Diamond na Ally Kiba kwamba wako kwenye beef, >> ‘Wasanii wa Tanzania tuna wapambe na sio marafiki kwa sababu mpambe unaweza kuwa umelewa yeye ndio anakoleza ugomvi lakini rafiki ni yule anaekuonya au kukushauri’

‘Ninachowashauri hawa wadogo zangu watulie chini wajitambue ni Wasanii na usanii wao ni wa kutengeneza pesa, tena watengeneze hata Tour ya Amani wazunguke nchi nzima.. wazunguke hata Afrika Mashariki na sio hizi beef’

Kwenye sentensi nyingine Dudubaya amesema ‘kuna gazeti moja liliandika eti Diamond alihonga hela kuchukua hizo tuzo, ni vitu vya kipumbavu kabisa… hujui kusoma lakini picha lazima uione, Ali Kiba na Diamond kila mmoja ana mama yake, wakae chini kama binadamu wajitambue, waachane na mambo ya watoto wa hapa mjini hawa ni wapambe tu mwisho wa siku hawana msaada
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni