Jumanne, 1 Julai 2014
FORBES: Beyonce ndiye Cerebrity mwenye nguvu 2014
Mwanamuziki wa Marekani Beyonce, ambaye pia ni mke wa rapa Jay Z ametajwa na jarida la Forbes kuwa ndio mtu maarufu mwenye nguvu kwa mwaka 2014.
Jarida maarufu la Forbes limemtaja Beyonce kuwa msanii mwenye nguvu kwenye orodha ya watu mashuhuri tangu ajitambulisha mwaka 2004.
Mwimbaji huyo, ambaye alijiingizia dola za kimarekani milioni 115 mwaka uliopita, aliungana na mumewe aliyeshika nambari 6, ambaye alitengeneza dola za kimarekani milioni 60.
Wawili hao wapo pamoja kwenye ziara nchini Marekani, inayojuliakana kama”On the Run”.
Forbes hutoa wasanii 100 kwa kuangalia majina yao, na kuangalia yametajwa kiasi gani katika magazeti, televisheni na redio. Pia huangalia nguvu walizonazo kwenye majukwaa 11 ya mitandao ya kijamii, ikiwemo Twitter, Facebook na YouTube.
Mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James ameshika nafasi ya pili kwenye orodha ya mwaka hu, huku nyota wa hip hop Dr Dre akishikilia nafasi ya tatu.
Oprah Winfrey, ambaye alishika nafasi ya kwanza mwaka uliopita, ameshika nafasi ya nne.
Forbes wamekuwa wakitoa orodha ya wasanii 100 kila mwaka kwa miaka 15b iliyopita.
Madonna, David Beckham, Tom Cruise na Adam Sandler ni miongoni mwa nyota walioshuka kwenye hesabu ya mwaka huu.
Orodha kamili;
1. Beyonce Knowles – $115m
2. LeBron James – $72m
3. Dr Dre – $620m
4. Oprah Winfrey – $82m
5. Ellen DeGeneres – $70m
6. Jay Z – $60m
7. Floyd Mayweather – $105m
8. Rihanna – $48m
9. Katty Perry – $40m
10. Robert Downey Jr – $75m
2. LeBron James – $72m
3. Dr Dre – $620m
4. Oprah Winfrey – $82m
5. Ellen DeGeneres – $70m
6. Jay Z – $60m
7. Floyd Mayweather – $105m
8. Rihanna – $48m
9. Katty Perry – $40m
10. Robert Downey Jr – $75m
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni