Sports and Entertainment

Jumatano, 23 Julai 2014

Kama unamchukia Cristiano Ronaldo usisome hii story ,,, kitakukukera alichokisema

Hakuna maoni :

Staa wa Ureno pamoja na klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo 29, amedai kuwa hanampango wa kustaafu soka kwasasa na labda atalifikiria jambo hilo miaka sita au saba ijayo na kusisitiza kuwa mpango wake wa msimu mpya wa  2014/2015 ni kuhakikisha anapata tuzo zakutosha

‘Kwasasa sina mpango wakustaafu, najisikia nipo vizuri kiafya hata majeraha yaliyokuwa yananitesa msimu uliopita kwasasa nimepona kwa 100%,
‘Japokuwa msimu uliopita sikuwa fiti kwa 100% lakini tuliweza kupata mataji makubwa kama Uefa Champions League na Copa del Rey naamini kwa kikosi tulichonacho kwa msimu unaokuja tunaweza tukachukua hata makombe  sita’
Aliyasema hayo katika moja ya sherehe zilizoandaliwa na wadhamini wa klabu ambapo ‘party’ yenyewe ilifanyika katika Jiji la Tokyo nchini Japan
Kwasasa hivi kikosi ya Real Madrid ipo nchini Marekani kujifua kwa ajili ya msimu ujao lakini mastaa kama Cristiano Ronaldo, Sergio Ramos, Toni Kroos, Varane, Sami Khedira,
Angel Di Maria, Karim Benzema, Luka Modric, Marcelo,na Iker Casillas wote hao watajumuika na kikosi kilichopo Marekani tarehe 26 julai
Baada ya kuruhusiwa kuendelea na likizo zao mara baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia nchini Brazil
Kikosi hicho kitajipima uwezo nchini Marekani na timu za Manchester United, Inter milan na As Roma kati ya tarehe 27 julai na tarehe 2 Agosti
 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni