Jumamosi, 26 Julai 2014
Van Gaal akutana na Fergie
Louis van Gaal atakaa kitako na Sir Alex Ferguson kwa mara ya kwanza mwishoni mwa juma wakati kocha huyo wa zamani wa Manchester United atakapojiunga na timu hiyo mjini Washington.
Kocha huyo mpya wa United alisema wiki iliyopita kwamba alitamani kunywa kahawa na Ferguson na anaelewa kuwa anahitajika kuchukua akili za gwiji huyo wa Old Trafford kwa ajili ya maisha ya Old Trafford.
Fergie amekuwa mapumzikoni kwa muda ila anasafiri kwenda Marekani leo Jumamosi na atakuwa kwenye sherehe za United mjini Washington na kisha Detroit.
Mskochi huyo ataungana na wanachama sita wa familia ya Glazer ambao wataungana na ziara ya United ambayo ina watu wapatao 170 nchini Marekani.
United ambao wameanza vizuri mjini Los Angeles kwa kuifunga LA Galaxy 7-0 huku wakijiandaa kucheza na Roma mjini Denver leo mchana.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni