Jumapili, 6 Julai 2014
MILIO YA RISASI YARINDIMA LAMU
Kumekuwa na milio ya risasi katika mji wa Lamu nchini Kenya.
Mwandishi wa BBC Dennis Okari anasema nyumba zimechomwa moto katika
eneo la Hindi, karibu na mji wa Mpeketoni. Kituo cha polisi pia kimeshambuliwa katika eneo la Gamba.
Kituo cha maafa cha Kenya kimesema kupitia Twitter kuwa polisi wamekwenda kushughulikia tukio hilo.
Haifahamiki nani amehusika na tukio hili, lakini kundi la al-Shabab limekuwa likifanya mashambulio kadhaa katika eneo hilo.
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema limepeleka wafanyakazi wake wa shughuli za dharura, na hakuna taarifa zozote mpaka sasa za vifo au majeruhi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni