Alhamisi, 3 Julai 2014
MUGABE AWASHUKIA WAZUNGU
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewataka wakulima wazungu waliosalia nchini humo kutoa mashamba hayo kwa watu weusi.
"Tunasema hapana kwa wazungu wanaomiliki ardhi yetu, lazima waondoke," Bwana Mugabe amewaambia wafuasi wake kwenye mkutano wa hadhara.
Chama cha wakulima wazungu kimesema kinasikitika mvutano wa rangi unaibuka tena.
Wakosoaji wa rais huyo wanasema sera yake ya kuchukua mashamba yanayomilikiwa na wazungu ilisababisha kuporomoka kwa uchumi kuanzia mwaka 2000 hadi 2009.
Bwana Mugabe,90, ametawala Zimbabwe tangu uhuru mwaka 1980.
Mchambuzi wa BBC wa Zimbabwe, Stanley Kwenda anasema matamshi ya Bwana Mugabe yanashangaza, kwa kuwa serikali ilimaliza rasmi mpango wake wa mabadiliko ya sera ya ardhi karibu miaka miwili
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni