Jumapili, 27 Julai 2014
Real Madrid wanatisha sana wakiwa na Perez
Moja ya jambo la ajabu lililoonekana Bernabeu siku ya Jumanne ni pale Real Madrid walipotoa pauni milioni 60 kumsajili James Rodriguez na hivyo kukumbusha mwaka 2003 wakati kiongozi wa michezo Jorge Valdano alipomuambia rais Florentino Perez kuhusu kumsajili nyota wa Sao Paulo Kaka, 21.
Valdano alisema kuwa Kaka atamgharimu pauni milioni 7 ila ndani ya miaka minne atakuwa amemtengenezea euro milioni 40.
Perez alimwambia Valdano: “Utarudi kwangu endapo watataka pauni milioni 40 na tutamnunua.”
Umuhimu wa Perez ambaye amekuwa falsafa ya Galactico, ni kwamba hanunui mchezaji ambaye hajawahi kumsikia, unanunua nyota ambao wataujaza uwanja na kuwafanya wafadhili kukimbilia mlango mwako.
Anasema: Atagharimu zaidi, ila atatengeneza pesa zaidi baada ya kumsajili.
Orodha ya wachezaji walionunuliwa ghali na Real Madrid;
Gareth Bale: £86m
Cristiano Ronaldo: £80m
James Rodriguez: £60m
Kaka: £56m
Zinedine Zidane: £45m
Luis Figo: £37m
Ronaldo de Lima: £34m
Karim Benzema: £30m
Xabi Alonso: £30m
Luka Modric: £30m
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni