Katika miezi ya hivi karibuni hasa katika mitandao ya kijamii kumeibuka mtindo wa kupiga uitwao selfie - ambapo mtu hutumia camera ya mbele ya simu au digital camera kujipiga picha mwenyewe.
Mtindo huu wa upigaji picha ambao umeshika hatamu sasa duniani kote umemuingiza matatizoni mhudumu mmoja wa mgahawa huko Barbados.
Kyson Forde, mhudumu wa mgahawa wa Cliff, amefukuzwa kazi baada ya kupiga picha ya ‘selfie’ na mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Robin van Persie.
Kilichosababisha kufukuzwa kwa Kyson ni katazo la mgahawa huo kwa wafanyakazi wake kutotumia simu za mkononi kwenye sehemu ya kulia chakula.
Chanzo cha habari kinaeleza kwamba RVP akiwa na familia yake kwenye mgahawa huo, alifuatwa na Keyson ambaye ni shabiki mkubwa wa Man Utd na kuombwa kupiga selfie, akafanikiwa na kisha akaitundika kwenye mitandao ya kijamii.
Waajiri wake walipoona ajira yake ikaingia ruba.
Van Persie yupo Barbados mapumzikoni baada ya kuiongoza timu yake ya taifa Uholanzi kushika nafasi ya 3 kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni