Ijumaa, 25 Julai 2014
TETESI ZA USAJILI MAJUU
Kiungo wa Juventus Arturo Vidal ameipa pigo Manchester United kwa kudai hatokwenda Old Trafford (Daily Mail), Liverpool watatumia madai hayo kumfuatilia kwa makini Vidal kwa kutoa pauni milioni 42.5 (Metro), Atlètico Madrid wameanza kumfuatilia mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, 26 (Times), kiungo wa Chelsea Marko Marin, 25, anazungumza na Besitkas kwenda kwa mkopo (Sun), meneja wa Aston Villa,, Paul Lambert amesema nahodha wake Ron Vlaar, 29, anayefuatiliwa na Tottenham, hauzwi (Sun), beki wa Spurs Vlad Chiriches huenda akaenda Roma (Sun), Jose Mourinho anakaribia kukamilisha uhamisho wa Didier Drogba, 36, huku kipa Petr Cech, 32, akimuonya Mourinho kutomkalisha bench msimu ujao (Sun), Arsenal wanamfuatilia kipa wa Real Madrid Iker Casillas, 33, na wamempa mkataba wa miaka mitano kwa mshahara wa pauni milioni 1.4 kwa mwaka (Daily Express), Manchester United wanapanga kumfuatilia Memphis Depay, 20 wa Uholanzi (Sun), Per Mertesacker, 29, Mesut Ozil, 25 na Lukas Podolski, 29, watakosa mwanzo wa msimu baada ya kuongezewa likizo kufuatia kushinda Kombe la Dunia (Daily Mirror), Ryan Giggs amemuelezea meneja mpya wa Manchester United Louis van Gaal, kama "Alex Ferguson Mpya" (Telegraph), nahodha wa Liverpool Steven Gerrard, 34, anajiandaa kusaini mkataba wa mwaka moja zaidi (Liverpool Echo), Inter Milan imedai inakaribia kumsajili beki Gary Medel wa Cardiff City (Wales Online), Sunderland wana matumaini ya kumsajili beki wa Chelsea Patrick van Aanhold (Metro), Arsenal wanamtazama kwa karibu Douglas Costa ambaye amekataa kurudi Shakhtar Donetsk kutokana na matatizo ya kisiasa. Mchezaji huyo anafuatiliwa pia na AC Milan na Spurs (Sky Sport Italia), Arsenal wanajiandaa kuwasilisha maombi yao kwa Hoffenheim kumsajili Roberto Firmino. Mshambuliaji huyo kutoka Brazil anatakiwa pia na Inter Milan (Tuttomercatoweb.com) matumaini ya Manchester United kumsajili Juan Cuadrado yameongezeka baada ya Bayern Munich kuacha kumfuatilia mchezaji huyo wa Fiorentina (talkSPORT).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni