Ijumaa, 25 Julai 2014
Wanawake vijana walalamikia vikwazo katika fani ya muziki
Vijana wa kike wenye vipaji vya fani ya muziki wamelalamika kupata vikwazo na usumbufu mkubwa wanapotaka kutumia fani yao kujitolea kusaidia jamii hali inayowakatisha tamaa na wameziomba idara zinazohusika kuwasaidia kuondoa changamoto hizo.
Mmoja wa vijana hao Bi. Lidiya Mchaina amesema licha ya tatizo hilo kuwaathiri vijana wote ni kubwa zaidi kwa vijana wa kike na linahitaji kudhibitiwa kwani licha ya kukwamisha jitihada za vijana wa kike za kujinasua na utegemezi na pia umaskini ni unyanyasaji wa kijinsia.
Akizungumzia malalamiko hayo mmbunge wa jimbo la Arusha Mh Godbless Lema ambaye amekutana na baadhi ya vijana hao amesema atafuatilia na amewataka kutokata tamaa na kwani hakuna kisichowezekana na pia wasichoke kutoa taarifa za changamoto zinazowakabili kwani hakuna kilicho rahisi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni