Sports and Entertainment

Jumapili, 6 Julai 2014

Watu wanaoongoza kwa kuchukiwa

Hakuna maoni :

Katika maisha kuchukiwa ni jambo la kawaida na huwa linatokea kwa kila mtu, lakini kulingana na uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandao wa Rumorfix, umeweza kutoa orodha ya majina kumi ya watu mashuhuri wa marekani wanaoongoza kwa kuchukiwa hasa kutokana na vitendo wanavyofanya au walivyowahi kufanya kuonekana kutoipendeza jamii kwa namna moja ama nyingine.
Nafasi ya kwanza ikikamatwa na aliyekuwwa mmiliki wa timu ya mpira wa kikapu ya Los Angels Clippers, Donald Sterling, kwa kiwango cha asilimia 92, hiyo ni kutokana na dhambi ya ubaguzi aliyomfanyia kimada wake,  hali iliyopelekea idadi kubwa ya watu weusi kumchukia.

(1).  DONARD STERLING – 92%
Donald Sterling
(2).  BERNARD MADOFF - 90%
Bernard Madoff
Nafasi ya Pili inashikiliwa na Mchumi, mshauri wa masula ya uwekezaji na mwenyekiti wa NASDAQ, BERNARD MADOFF
(3).  O. J.” Simpson - 88%
O. J Simpson
Nafasi ya Tatu inakamatwa na Muigizaji, Orenthal James “O. J.” Simpson AKA The Juicy
(4).  CONRAD MURRAY -  88%
Conrad Murray
Aliyekuwa Daktari wa Michael Jackson, Conrad Murray anakamata nafasi ya nne, huku shutma za kuhusika na kifo cha Mfalme huyo wa Pop Dunia zikichangia kwa kiasi kikubwa kuchukiwa na wafuasi wa nyota huyo
(5).  JUSTIN BIEBER -  86% 
Justin Bieber
Msanii wa Muziki toka nchini Canada, Justin Bieber amekamata nafasi ya tano, sababu kubwa ikitajwa ni kuharibu vijana wadogo kutokana na mfumo mzima wa maisha anaoishi hali iliyyopelekea atake kufukuzwa nchini Marekani kutokana na vitendo vya uvunjaji wa sheria
(6). PHIL SPECTOR  -  83%
PHIL SPECTOR
Mtayarishaji mkongwe wa muziki na mtunzi wa nyimbo
(7).  AARON HERNANDEZ  -  81%
The heavily inked Aaron Hernandez
Wamerekani weusi hawatoweza kumsahau mchezaji huyu wa Amerika Football baada ya kudaiwa kuhusika kupanga mauaji ya mchezaji mwenzake, Odin Lloyd aliyekutwa amefariki nje ya nyumba yake

(8). MICHAEL LOHAN  -  76%
MICHAEL LOHAN
Baba mzazi wa Lindsay Lohan na Ali Lohan

(9).  ELIOT SPITZER  -  73%
Eliot Laurence Spitzer
Gavana wa zamani wa New York
(10).  JON GOSSELIN  -  71%
JOS GOSSELIN

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni