Sports and Entertainment

Jumanne, 22 Julai 2014

X VS Y!!! DIAMOND VS ALI KIBA : BIFU AMBALO WAANDISHI WA HABARI WANALIPENDA , HABARI AMBAYO MASHABIKI WANAIOGOPA

Hakuna maoni :


Unawajua hao katuni hapo juu?


Katuni hao hapo juu wanasumbua akili za watu Ulimwengu mzima , kila mtu amekuwa na jibu lake na hakuna jibu sahihi, kati ya watu kumi watano wapo kwa huyu katuni wa kushoto na watano wapo kwa huyu katuni mwingine, Dunia imekosa jibu , wabishi na wabishani wameshindwa, magwiji wamechemka, wachunguzi hawana majawabu,viwanja havina majibu na mbaya zaidi takwimu zimeshindwa kuamua nani ni nani kati yao na hilo ndilo swali linaloumiza kichwa watu wote Duniani ikiwemo mimi mwenyewe.


#10Lionel Messi,  Barcelona, Adidas,Argentina,

#7Cristiano Ronaldo,Real Madrid,Nike,Portugal,

Dunia imeshuhudia kwa mara nyingine ubishani juu ya watu wenye vipaji vinavyolingana kiasi cha kuchanganya na kugawa mashabiki pande mbili ,,,



baada ya miaka kadhaa ya kukosa majibu nani mkali kati yao Dunia imebaki kimya bila jawabu hii inatokana na vipaji visivyo vya kawaida vya kusakata kabumbu walivyojaaliwa

Kwetu Tanzania tuna shida lakini hii bahati nzuri au mbaya haipo kwenye soka pengine ingeleta mzozo mkubwa na ugomvi, hii ni katika masuala ya burudani,

Kila mtu Tanzania anajisemea moyoni sasa"ugomvi nilikua sitaki utokee umetokea"


Hawa ni magwiji wa muziki wa bongo fleva , wafalme wasiopikika chungu kimoja, mafahari wawili , Ali Kiba na Diamond Platnumz,
mpaka leo hii hakuna alieamini kama vijana hawa wenye vipaji na sauti tishio nchini kama wanaweza kutofautiana, mbaya zaidi wote wanatokea katika mkoa wa kigoma
Tanzania ikiwa kimya bila mtu yoyote kushadadia upande wowote , kumebaki na maswali juu ya chanzo cha ugomvi na tofauti zao



ALI SALEH KIBA
huyu ni kipenzi cha mashabiki wote daima akijulikana kwa usiri na upole wake ,kipaji cha sauti alichonacho ndicho kilimuacha hoi nguli wa muziki wa R n B ,Duniani , R.kelly na kumpa nafasi ya kuanza kuimba katika nyimbo ya umoja wa wasanii wa africa aliyokua akiisimamia ijulikanayo kama One 8

Watu wengi wanampenda , amebaki mioyoni mwa watu na daima amekua kimbilio la chipukizi
amekua kimya sana lakini uwezo wake hauna shaka atarudi na balaa zake


NASEEB ABDUL

Huyu hapa mfalme mwingine wa muziki wa Bongo flava, gwiji ambaye habari yake imesambaa Dunia nzima , kama Tanzania ina madini mengi hili ni dini la kujivunia sana , sauti yake na jina lake ni habari kuu kila leo magazetini, wapenzi wake ,maisha yake,familia yake,nyumba yake vimekua havina vificho kutokana na ukweli kwamba ana mvuto wa kipekee


DIAM0ND PLATNUMZ NA ALI  KIBA habari ya ugomvi wao inashtua wengi mno lakini kadiri magazeti yanavyoendelea kuripoti bifu hili la gumzo, mashabiki wameziba masikio hawataki ugomvi huu kuusikia kutokana na ukweli kuwa hawa ni watu wanaopendwa na kuheshimika na rika na makundi yote Tanzania

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni