Ijumaa, 1 Agosti 2014
EBOLA YAZIDI KUTIKISA, WATU 57 ZAIDI WAFARIKI
Israel imesema haitaondoa majeshi yake kutoka Gaza hadi pale itakapomaliza kazi ya kuharibu mfumo wa njia za chini ya ardhi , licha ya shutuma kazi kutoka Umoja wa Mataifa kuhusiana na idadi ya vifo vya raia wa Kipalestina. Akizungumza katika mkutano maalum wa baraza la mawaziri mjini Tel Aviv, waziri mkuu Benjamin Netanyahu amesema hatakubali hatua yoyote ya kusitisha mapigano ambayo haitaruhusu majeshi yake kuendelea kuharibu mfumo wa mahandaki hayo ya wapiganaji yanayotumiwa kushambulia ardhi ya Israel.
Wakati huo huo baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao cha dharura kuhusu Gaza baada ya shambulio dhidi ya shule katika ukanda wa Gaza. Mkuu wa idara ya misaada ya dharura ya Umoja wa mataifa Valerie Amos amesema kuwa pande zote mbili Israel na Hamas zinapaswa kuangalia sheria na kanuni za mapigano.
Ametaka pande hizo kuchukua hatua ya kusitisha mapigano kwa muda ili kutoa misaada kwa watu wanaohitaji misaada hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni