Jumatano, 6 Agosti 2014
Marekani kuwekeza zaidi Afrika

Marekani imepanga kuongeza uwekezaji wake barani Afrika ili kuizidi China inayoonekana kuja kwa kasi kiuchumi na kiuwekezaji Afrika.
Makampuni ya Marekani yameahidi kuweka kiasi cha dola bilioni 14 barani Afrika kwenye maeneo ya nishati na miundombinu, alisema Rais wa Marekani Barack Obama.
Tangazo hilo lilitolewa kwenye Mkutano wa Viongozi wa Afrika na Marekani, ambao ulihudhuriwa na zaidi ya viongozi 40 wa mataifa ya Afika.
Mkutano huo ni jitihada ya kuimarisha mshikamano wa Marekani na Afrika baada ya China kuongeza uwekezaji barani Afrika.
Obama pia aliwaandalia chakula cha jioni Viongozi wa Afrika kwenye ikulu ya White House.
Mpango huo ulitangazwa siku ya Jumanne ulihusisha ushirikiano wa dola bilioni 5 na kampuni binafsi za Blackstone na Aliko Dangote, ambaye ndiye mfanyabiashara tajiri Afrika, kwa ajili ya mradi wa uzalishaji nishati Kusini mwa Jangwa la Sahara, vile vile uwekezaji zaidi wa mradi wa Obama wa Power Afrika Initiative.
Kwa mujibu wa White House, Power Africa ilipokea ongezeko la dola bilioni 12 kama ahadi dhidi ya jitihada za kuendeleza usambazaji wa nishati barani Afrika kupitia ushirikiano wa wawekezaji na taifa husika.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni