Jumamosi, 2 Agosti 2014
Mourinho : nyie!! huyu Costa noma
Jose Mourinho anadai wachezaji wa Chelsea wanashangazwa na uwezo wa Diego Costa, kwamba mshambuliaji huyo wa Hispania ndio mchezeshaji wa timu ambaye timu hiyo ilimkosa mbele misimu kadhaa iliyopita.
Costa, aliwasili Stamford Bridge kwa ada ya pauni milioni 31 akitokea Atletico Madrid, amemvutia kocha wa Chelsea mpaka sasa kwenye mechi za maandalizi ya ligi, akifunga goli katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Olimpija Ljubljana wiki iliyopita.
Mhispania huyo alifunga magoli 36 katika mechi 52 za mashindano ya msimu uliopita akiwa Atletico Madrid, ila Mourinho anasisitiza kuwa ni zaidi ya mfungaji magoli.
Mourinho aliiambia Sky Sports kuwa: “Ana mchango mkubwa sana kwetu. Ni mchezaji mahiri. Kimbinu pia ni mzuri, mzuri sana.
“Ndio mana wachezaji wengi wanamfurahia na wanashangazwa naye, kwa sababu ya uwezo wake mkubwa kuliko tulivyotegemea.”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni