Jumamosi, 2 Agosti 2014
tetesi za usajili majuu
Barcelona wanajiandaa kutibua mpango wa Manchester United, kwa kumnyakua kiungo kutoka Colombia, Juan Cuadrado, 26, kutoka Fiorentina (Daily express),
hata hivyo Man U wanadaiwa kutoa dau la pauni milioni 55 sawa na PSG ili kumshawishi winga huyo (Metro)
, mashambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 29, amesema katika soka chochote kinaweza kutokea na huenda kuna uwezekano wa kurejea Old Trafford (Manchester Evening News),
meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini ameambiwa beki wa Porto Eliaquim Mangala, 23, atakuwa mchezaji wa mwisho kusajiliwa msimu huu (Times),
Barcelona na Brondby ya Denmark wanafikiria kumchukua beki wa kati wa Liverpool Daniel Agger, 29, kufuatia kuwasili kwa beki Dejan Lovren kutoka Southampton (Daily Mail),
Arsenal wapo tayari kumsajili beki wa zamani wa Liverpool Alvaro Arbeloa, 31, kutoka Real Madrid, iwapo Thomas Vermaelen, 28, ataondoka Emirates (AS), Manchester United wapo tayari kumsajili Vermaelen kwa pauni milioni 12, licha ya kuwa beki huyo ni majeruhi baada ya kuumia wakati wa Kombe la Dunia akiwa na Ubelgiji (Guardian),
Liverpool wamepata kikwazo katika jaribio lao la kumsajili mshambuliaji Ezequiel Lavezzi kutoka PSG, baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina kutaka kwenda Juventus (Daily Express),
boss wa Newcastle Alan Pardew amesema amekata tamaa kumfuatilia Loic Remy, 27, kutoka QPR (Newcastle Chronicle)
, West Ham wanajiandaa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Stoke City Peter Crouch, 33, kuimarisha safu ya ushambuliaji baada ya Samuel Eto'o kushindwa kuafikiana na Upton Park (Daily Star)
, kipa wa Southampton Artur Boruc, 34, ananyatiwa na Bayern Munich (Telegraph),
Liverpool 'watawasaidia' Manchester United katika mchakato wao wa kumsajili Mats Hummels, 25, kwa kumruhusu beki wao Tiago IIori, 21, kwenda Borussia Drotmund kwa mkopo (Daily Star),
Everton na Norwich wanataka kumsajili mshambuliaji kutoka Gambia Modou Barrow, 21, anayechezea Ostersunds FK (Sky Sports),
Tottenham wanafanya mazungumzo na beki kutoka Argentina, Mateo Musacchio, 23, anayechezea Villareal. Mchezaji huyo alihusishwa na kwenda Barcelona pia (Daily Mirror),
QPR wanafikiria kumchukua kiungo Mauricio Isla, 26, kutoka Juventus kwa mkopo (Daily Mail),
mshambuliaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor, 30, ataanza mazoezi siku ya Jumamosi lakini anasema alijisikia dhaifu sana baada ya kupata malaria mwezi Juni hakuweza hata kutembea (Sun)
, kocha wa Real Madrid, na meneja wa zamani wa Chelsea, Carlo Ancelotti amesema itakuwa "vigumu" kwa Louis van Gaal kuibadili Manchester United na kuwa timu inayowania ubingwa msimu huu (Guardian),
kiungo wa England Ashley Young, 29, yuko tayari kucheza kama 'beki-winga' ili kufufua matumaini yake chini ya meneja mpya Van Gaal (Daily Mirror),
meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ametabiri kuwa ushindani utakuwa mkali sana msimu huu kutokana na sheria mpya za usawa wa kifedha ambazo zitawaathiri mahasimu wa Arsenal (Times)
kipa wa zamani wa Chelsea Mark Bosnich anaamini Petr Cech, 32, ataondoka Darajani msimu huu, iwapo atakuwa namba mbili nyuma ya Thibaut Courtois, 22, (Talksport),
mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, 25, ametoa onyo kwa mahasimu wa Arsenal, kupitia twitter akisema "wamwangalie sana" Alexis Sanchez akisema atakuwa hatari. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na Jumamosi njema- Cheers!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni