Jumamosi, 2 Agosti 2014
TETESI ZA USAJILI MAJUU
Arsenal wameambiwa Juan Quintero, 21,
Manchester United wanakaribia kufanikisha uhamisho wa pauni milioni 20 wa Mats Hummels, 25, huku Borussia Dortmund wakiwa na matumaini ya kuziba pengo hilo kwa kumchukua Tiago IIori, 21, kutoka Liverpool kwa mkopo (Daily Mirror)
, rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amethibitisha kuwa klabu yake inamtaka kiungo wa Manchester United Marouanne Fellaini, 26, ingawa kuna wachezaji wengine pia inawafuatilia (Daily Telegraph)
, Liverpool inatazama kuwachukua mabeki kutoka Spain Alberto Moreno, 22, wa Sevilla na Javier Manquillo, 20 kutoka Atletico Madrid (Daily Star),
West Ham wamekuwa na mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o, 33, na pia Hugo Almeida, 30 kutoka Besitkas (Times),
kocha wa Atletico Madrid Diego Simione yuko tayari kupanda dau kumchukua kiungo wa Manchester United Shinji Kagawa, 25 (Daily Express)
, QPR wameelekeza macho yao kumfuatilia kiungo Morgan Amalfitano, 29 kutoka Marseille, aliyeichezea West Brom kwa mkopo msimu uliopita (Daily Mail),
Arsenal wanamfuatilia beki wa Real Madrid Alvaro Arbeloa iwapo Thomas Vermaelen ataondoka Emirates (AS), Arturo Vidal wa Juventus amepita katika vipimo vya afya na anasubiri makubaliano ya mwisho kusaini mkataba na Manchester United (Metro),
kiungo wa Porto Juan Quintero amesafiri kwenda London kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Arsenal (Marca). Share tetesi hizi na wapenda soka wote.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni