Jumamosi, 2 Agosti 2014
WAKATI DUNIA NZIMA IKIUNDA KAULI MBIU "FREE GAZA" MAREKANI YAJIPANGA KUILINDA ISRAEL
Marekani imepitisha mswada unaotoa msaada wa kifedha kwa Israel kuimarisha mfumo wake wa kujilinda dhidi ya makombora.
Mswada huo unatoa dola millioni mia mbili na ishirini na tano kuimarisha mfumo huo ambao umetumiwa kuyatungua makombora kadhaa ya roketi kutoka kwa wapiganaji wa kipalestina katika majuma ya hivi karibuni.
Mpango huo wa fedha hatahivyo ni sharti upitishwe na bunge la wawakilishi na kutiwa sahihi na rais Obama.
Waandishi wanasema kuwa wabunge wa Marekani wamekuwa wakiunga mkono Israel hivyobasi mswada huo huenda usikabiliwe na vikwazo vyovyote.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni