Sports and Entertainment

Ijumaa, 1 Agosti 2014

Wenger ana wasiwasi Vermaelen anaweza kuondoka

Hakuna maoni :
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema huenda nahodha wake Thomas Vermaelen akaondoka Emirates.
Mchezaji huyo aliyekuwa kwenye kikosi cha Ubelgiji katika Kombe la Dunia 2014 amehusishwa na kuhamia Manchester United.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa, Wenger amesema Vermaelen ni majeruhi lakini amekiri: "Kuna uwezekano akaondoka."
Vermaelen aliyejiunga na Arsenal kutoka Ajax Juni 2009, alicheza mara 14 msimu uliopita katika mechi za Ligi Kuu.
Wenger amesema iwapo Vermaelen ataondoka, klabu hiyo itatafuta mtu wa kuziba pengo, kwa sababu mchezaji huyo "ni muhimu katika kikosi".
Ameongeza kuwa bado hajamaliza kufanya usajili, licha ya kusajili wachezaji wanne mpaka sasa.
Kocha huyo Mfaransa tayari amewasajili Calum Chambers, Alexis Sanchez, Matheiu Debuchy na David Ospina.
"Nimefurahi kwa sababu nimefanya kile nilichotaka kufanya, na bado nina imani ya kufanya zaidi," amesema.
"Ni tarehe 1 Agosti na dirisha la usajili linafungwa tarehe 31. Ni muda mrefu. Tuko mbele kidogo ya kawaida yetu kwa sababu soko ni kubwa kuliko ilivyokuwa zamani."
Wenger ameongeza kusema hatomsajili kiungo wa Porto Juan Quintero, ambaye amehusishwa na kuhamia Emirates.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni