Jumanne, 28 Oktoba 2014
PICHA : UKAWA WALIVYOLITIKISA JIJI LA DAR ES SALAAM

Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakionesha hati za waraka walizotiliana saini za ushirikiano katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , akihutubia kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dk. Emanuel Makaidi akihutubia kwenye hafla hiyo kabla ya kutiliana saini waraka wa ushirikiano.

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lisu (kulia), akimkaribisha Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jusa Ladhu, kuzungumza katika mkutano huo.

Makatibu wakuu wa vyama vinavyuunda Ukawa, wakionesha ishara ya mshikamano baada ya kusaini waraka huo wa ushirikiano. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrord Slaa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalimu, Seif Sharifu Hamad na Katibu Mkuu wa Chama NLD, Tozi Matwange.

Wafuasi wa ukawa wakionesha vidole vitatu juu wakimaanisha kuikubali serekali tatu inayotakiwa na Ukawa.

Vijana wa chama cha chadema wakiwa juu ya gari wakifuatilia matukio mbalimba yaliyokuwa yakiendelea uwanjani hapo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni